IQNA

Mashindano ya Qurani ya Dubai yaendelea

15:42 - August 23, 2010
Habari ID: 1979613
Mashindano ya Kimataifa ya Qurani Tukufu ya 'Zawadi ya Dubai' yanaendelea leo Jumatatu ambapo washiriki 7 kutoka Uingereza, Tunisia, Oman, Uzbekistan, Visiwa vya Comoro na Gambia watashindana.
Habari zaidi zinasema jana Jumapili ilikuwa siku ya tano ya Mashindano hayo ambapo washiriki kutoka nchi mbali mbali za dunia walishindana katika Ukumbi wa Biashara na Viwanda wa Dubai. Mashindano ya Kimataifa ya Qurani Tukufu ya 'Zawadi ya Dubai' yanatazamiwa kuendelea hadi tarehe 20 ya Mwezi Mkutufu wa Ramadhani.
Wakati huo huo Mohammad Amani Farani Naibu Mkuu wa Idara ya Konsuli ya Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Dubai amehudhuria Mashindano ya Kimataifa ya Qurani Tukufu ya 'Zawadi ya Dubai' na kusema: "Mashindano ya Qurani ya Dubai yana nafasi muhimu ya kuwahimiza vijana washindane katika uga wa kuhifadhi Qurani Tukufu'. Amesema washiriki Wairani waliweza kupata nafasi nzuri katika mashindano yaliyopita ya Qurani ya Dubai. Ameongeza kuwa, 'Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina mashindano mengi ya Qurani katika uga wa kitaifa na kimataifa na hili linaashiria umuhimu wa Qurani Tukufu katika jamii ya Iran".
639541
captcha