Kila mwaka wakati wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Dubai hufanyika uteuzi wa kuainisha Shakhsia wa Kiislamu, fahari ambayo mwaka huu imemwendea rais wa zamani wa Sudan.
Swar al Dhahab ambaye kwa sasa ni kiongozi wa Baraza la Wadhamini wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ulinganiaji wa Kiislamu, ametoa huduma kubwa kwa Uislamu, Waislamu na Qur'ani katika nchi mbalimbali duniani.
Kiongozi huyo wa zamani wa Sudan pia ameshiriki katika mikutano mingi ya kimataifa na kuandika makala nyingi kuhusu mbinu za kulingania Uislamu, changamoto zinazokabili ulinganiaji na kuwatambulisha wasiokuwa Wislamu misingi na mafundisho ya dini hiyo tukufu.
Kazi nyingine za shakhsia huyo wa Kiislamu ni pamoja na kufanya jitihda za kujenga zaidi ya misikiti 2000 katika nchi mbalimbali za Afrika na Ulaya mashariki, kushiriki katika ujenzi wa vituo 6 vya kulea mayatima katika nchi za Kiafrika na jitihada za kuasisi vituo vya Kiislamu, shule, zahanati na mahospitali kwa ajili ya Waislamu kwenye nchi maskini za Kiafrika. 640271