Kongamano la Kimataifa la Hija limepangwa kufanyika tarehe 26 na 27 za nwezi wa Septemba mjini Dar es Salaam Tanzania likisimamiwa na Kamati ya Hija ya Tanzania kwa ushirikiano wa Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu na Iran na mjumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania.
Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Iran nchini Tanzania Mustafa Ranjbar Shirazi ameiambia IQNA kwamba kongamano hilo la kimataifa litahudhuriwa na wawakilishi mia moja wa kamati za hija za nchi za mashariki mwa Afrika, mawaziri Waislamu na maafisa wa masuala ya hija wa nchi mbalimbali.
Ameongeza kuwa washiriki katika kongamano hilo la siku mbili watajadili na kuchunguza nafasi ya hija kati ya Waislamu, umoja wa umma wa Kiislamu kwa msaada wa hija, falsafa na misingi ya kimaarifa ya kuzuru nyumba ya Mwenyezi Mungu al Kaaba na matokeo ya kongamano hilo la kila mwaka.
Bwana Ranjbar amesema kuwa pambizoni mwa kongamano hilo kutafanyika maonyesho ya vitabu na vitu vingine vya kiutamaduni vinavyohusiana na ibada ya hija kama filamu na programu za kumputa. 644119