IQNA

14:51 - August 31, 2010
Habari ID: 1985414

Nchi za Kiislamu kutoa msaada wa dola bilioni moja kwa waathirika wa mafuriko Pakistan

Nchi za Kiislamu wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC zimeahidi kutoa msaada wa dola bilioni moja kwa waathirika wa mafuriko nchini Pakistan.

Nchi kama Uturuki, Saudi Arabia, Qatar, Kuwait, Umoja wa Falme za Kiarabu, wafanya biashara kadhaa wa Kiislamu na jumuiya zisizokuwa za serikali zimetuma barua ya pamoja kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu Ekmeleddin Ihsanoglu zikiahidi kutoa msaada wa dola bilioni moja kwa watu walioathiriwa na mafuriko nchini Pakistan.
Kwa upande wake Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa iko tayari kutuma misaada zaidi ya kibinadamu nchini Pakistan. Hadi sasa Iran imetuma shehena zenye tani 400 za misaada inayojumuisha mahema, vyakula, maji safi ya kunywa, blanketi na kadhalika kwa waathiriwa wa mafuriko huko Pakistan.
Zaidi ya watu milioni 20 wamelazimika kuhama nyumba zao nchini Pakistan kutokana na mafuriko makubwa yaliyoikumba nchi hiyo. Watu hao wanasumbuliwa na uhaba mkubwa wa chakula na maji safi na wanakabiliwa na hatari ya magonjwa ya kuambukiza. 645677


captcha