IQNA

Tamasha ya kila mwaka ya kuwatuza wahifadhi wa Qur'ani kufanyika Masjidul Haram

15:34 - September 01, 2010
Habari ID: 1985738
Tamasha ya kila mwaka ya kimataifa ya kuwatuza wahifadhi wa Qur'ani Tukufu ilifanyika jana Jumanne katika Msikiti wa Haram katika mji mtakatifu wa Makka.
Tamasha hiyo iliandaliwa na Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu ya mjini Makka. Kwa mujibu wa tovuti ya Tasbih, wanafunzi wa jumuiya iliyotajwa waliofanikiwa kuhifadhi Qur'ani nzima au juzuu 15 za kitabu hicho kitakatifu wametuzwa na kutunukiwa zawadi kutokana na juhudi zao hizo.
Nawaf bin Abdul Muttalib Aal Ghalib mkuu wa Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu amesema kwamba tamasha hiyo imeandaliwa kwa shabaha ya kuwashajiisha vijana kusoma na kuhifadhi Qur'ani na kwamba walimu wa Qur'ani 25 wa jumuiya hiyo ambao wamefanya juhudi kubwa za kufundisha kitabu hicho pia watatunukiwa zawadi.
Katika upande wa pili, Ofisi ya Uratibu wa Muongozo na Ulinganiaji kwa Walio Wachache ya Makka siku ya Jumatatu iliandaa sherehe maalumu za kuwakaribisha Waislamu wapya walioingia katika Uislamu hivi karibuni huko Makka. Katika sherehe hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Shuhadaa, Waislamu wapya wapatao 73 kutoka nchi tofauti za dunia walishukuriwa na kukaribishwa kwenye Uislamu. 645978
captcha