Imesisitiza kwamba siku hiyo itakuwa siku ya kutangazwa upya azma ya jamii ya mwanadamu ya uzingatia utu wa mwanadamu na amani ya kiuadilifu duaniani.
Kwa mujimu wa taarifa hiyo, haki za binadamu ni msingi muhimu katika dhati ya mwanadamu unaopasa kuimarishwa na kupewa fursa ya kukamilika. Taarifa hiyo imeashiria kudhulumiwa taifa la Palestina na kuongeza kuwa ardhi za Palestina ni nembo ya dhulma kubwa inayofanywa dhidi ya mwanadamu duniani. Imesema, inasikitisha kuona kwamba wale watu wanaodai kuwa wamestaarabika na kuheshimu haki za binadamu ndio haohao wanaunga mkono utawala haramu wa Israel katika kukandamiza na kukanyaga haki za kimsingi za taifa dhulumiwa la Palestina.
Imeendelea kusema, nchi hizo zinazotoa madai matupu ya kuheshimu haki za binadamu na hasa Marekani, si tu kwamba zinaunga mkono waziwazi ukandamizaji huo wa Wazayuni dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi bali zinachangia pakuwa katika jinai zinazotekelezwa na utawala huo haramu dhidi ya Wapalestina, ikiwemo jinai ya hivi karibuni kabisa ya utawala huo ya kushambulia na kuua wanaharakati waliokuwa katika msafara wa misaada ya kibinadamu kwa ajili ya wakazi wa Ukanda wa Gaza unaozingirwa na utawala huo ghasibu.
Jumuiya iliyotajwa imeashiria umuhimu wa kufanyika juhudi za kuimarisha amani ya kiuadilifu katika pembe mbalimbali za duniani na kuongeza kwamba jambo la kwanza linalopasa kufanyika kuhusiana na suala hilo ni kusimamishwa mara moja uungaji mkono wa wazi wa baadhi ya madola kwa ukandamizaji, unyama na ugaidi unaofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi katika ardhi zao unazozikalia kwa mabavu na sehemu nyinginezo za dunia, na kisha kufanyika jitihada za kurejesha haki za mataifa yanayodhulumiwa.
Mwishoni mwa taarifa yake, Jumuiya ya Kimataifa ya Amani ya Kiislamu imewataka wapigania amani, wapigania uhuru, serikali na mataifa yote duniani kushikamana na kushirikiana katika Siku ya Kimataifa ya Quds ili kutetea amani na kuondoa dhulma ulimwenguni kwa mujibu wa thamani za dini na tamaduni zao. Imewataka walimwengu wote kushiriki katika maandamano hayo ili kutangaza upya azma yao ya kutetea na kuheshimu thamani za kiutu na kiuadilifu duniani. 646117