Kwa mujibu wa gazeti la As Sharq, kongamano hilo limeandaliwa kwa himaya ya Kituo cha Ushauri wa Kifedha cha Qatar. Bw. Ghanim bin Saeed Ale Saeed Mkuu wa Baraza la Kiidara la Kituo cha Ushauri wa Kifedha cha Qatar amesema kongamano hilo litahudhuriwa na mawaziri wa fedha, wakuu wa taasisi za utafiti wa kifedha na uchumi wa Kiislamu na wakuu wa benki kuu na taasisi za kifedha za nchi za Kiislamu. Ameongeza kuwa kongamano hilo litachunguza uwekezaji wa Kiislamu na masuala ya kiuchumi duniani.
647114