Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Malaysia la Benama, karibu wanaharakati 50 wa Kiislamu wa chama cha Hizbu Tahriri Ijumaa iliyopita waliandaa maandamana huko Java nchini Indonesia kulaani mpango wa watu wenye chuki dhidi ya Uislamu nchini Marekani waliotangaza Septemba 11 kuwa eti ‘Siku ya Kimataifa ya Kuchoma Moto Qur'ani’!
Chama hicho cha Kiislamu kimesema Waislamu kote duniani ni lazima wakabiliane na kitendo hicho ambacho kinalenga kuumiza nyoyo za Waislamu.
Pendekezo la Makanisa ya kufurutu ada ya Marekani ya kutaka kukichoma moto kitabu kitakatifu cha Waislamu limekabiliwa na hasira za Waislamu na wasiokuwa Waislamu duniani kote.
647594