Kwa mujibu wa shirika la habari la Malaysia Bernama, Waziri Mkuu Najib Tun Razak amesema kuwa kamisheni hiyo inapasa kuingilia kati jambo hilo haraka iwezekanavyo ili kuzuia kuenea kwake nchini humo. Amesema, watu wanaofanya dharau hiyo wanapasa kufahamu kwamba jambo hilo linawachukiza mno Waislamu na kwamba kwa mujibu wa sheria za Malaysia hakuna mtu yoyote anayepasa kuandika makala za dharau dhidi ya shakhsia au dini zinazokubalika nchini humo.
Waziri Mkuu wa Malaysia ameongeza kuwa vyombo vyote vya habari vya nchi hiyo vinapasa kuendeshwa kwa njia ya kuwajibika na kutii sheria za nchi na kwamba wahusika wanapasa kuepuka kuandika mambo yanayowakera wenzao na hasa kuhusiana na suala la dini.
Amesema, watu wa jamii zote za nchi hiyo bila kujali dini zao wanapasa kutambua kwamba Malaysia ni nchi iliyo na sheria madhubuti kwa ajili ya kulinda utukufu wa Uislamu. 648598