Kwa mujibu wa tovuti ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kiislamu cha Malaysia kongamano hilo litakalokuwa na anwani kuu ya "Umoja, Kipaumbele cha Kwanza" linafanyikwa chini ya usimamizi wa Baraza la Wanachuo wa chuo hicho.
Malengo ya kongamano hilo yametajwa kuwa ni pamoja na kuongeza ujuzi kuhusu umuhimu na udharura wa umoja katika harakati za vijana Waislamu, kukuza vipawa vya wasomi, kuimarisha mawasiliano miongoni mwa wasomi Waislamu na vilevile kuchunguza masuala muhimu ya Ulimwengu kwa lengo la kutafuta suluhisho la matatizo ya Waislamu duniani.
Kongamano hilo pia litajadili masuala ya utambulisho wa vyuo vikuu vya Kiislamu na wanachuo wa nchi za Kiislamu. Fauka ya hayo washiriki pia watajadili mahitaji ya nchi za Kiislamu na Waislamu duniani katika uga wa teknolojia, uchumi na jamii. 648787