Kwa mujibu wa Iqna, katika ujumbe huo, harakati hiyo imewatakia Waislamu idi njema na kusema kuwa hiyo ni fursa kwao kuimarisha mapenzi, upendo na amani katika ulimwengu wa Kiislamu, jambo ambalo litawarahisishia njia ya kuelekea kwenye saada, utukufu, heshima na baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Ujumbe huo umesema kwamba mwezi wa Ramadhani umekuwa wakati wa kupitia Waislamu mtihani wa kuhakikisha kuwa wanafanya ibada kwa ikhlasi kwa lengo la kumridhisha Mwenyezi Mungu na kutumai kwamba wataweza kutekeleza kivitendo maishani mafundisho na faida zote walizopata katika mwezi huu mtukufu.
Mwishoni ujumbe huo umewatakia kheri na fanaka Waislamu na kutaraji kwamba Mwenyezi Mungu atatakabali ibada zao walizotekeleza katika mwezi huu na kuwabariki zaidi katika siku zijazo. 651610