IQNA

Obama asema kuichoma moto Qur'ani Tukufu ni kwa madhara ya Marekani

11:53 - September 12, 2010
Habari ID: 1991445
Rais Barack Obama wa Marekani ametoa wito wa kuvumiliana dini mbalimbali huku uamuzi wa kasisi mwenye chuki na Uislamu wa kijikanisa kidogo huko Florida nchini Marekani wa kutaka kuchoma Qur'an Tukufu ukiendelea kulaaniwa duniani kote.
Obama amesema kwamba wananchi wa Marekani wanapaswa kuhakikisha kwamba hawakabiliani wenyewe kwa wenyewe na kwa mara nyingine amekariri wasiwasi wake kuwa, kitendo hicho huenda kikahatarisha maisha ya askari wa Marekani walioko nje ya nchi hiyo.
Kasisi Terry Jones alikuwa ametishia kutekeleza kitendo hicho cha kishetani na kiwendawazimu Septemba 11 kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mashambulizi yaliyojaa utata yaliyotokea nchini Marekani mwaka 2001.
652323
captcha