IQNA

Kongamano la Dini na Umaanawi katika Jamii kufanyika mjini Chicago Marekani

11:47 - September 15, 2010
Habari ID: 1994441
Kongamano la kimataifa la Dini na Umaanawi katika Jamii limepangwa kufanyika tarehe 15 hadi 17 za mwezi Februari mwakani huko Chicago katika jimbo la Illinois nchini Marekani.
Kwa mujibu wa tovuti ya religioninsociet masuala muhimu yatakayojadiliwa katika kongamano hilo ni pamoja na tasisi za kidini, jamii ya kidini, masuala yanayofanana na yanayotofautiana kidini na siasa za kidini.
Kuhusiana na maudhui ya taasisi ya dini masuala kama vile thamani za kidini, vyanzo vitakatifu, falsafa ya kidini, akili na dini, mitazamo ya kale na ya kisasa kuhusiana na dini, elimu na dini, sheria na dini, dini na biashara na mitume wa Mwenyezi Mungu yatajadiliwa.
Kuhusiana na maudhui ya mambo yanayofanana na kutofautiana kidini masuala yanayohusu uratibu baina ya dini, mazungumzo baina ya dini, maelewano ya kidini, dini katika mfumo wa utandawazi, vitabu vitakatifu, uongozi tofauti wa kidini, kuelewa dini tofauti na mazungumzo baina ya dini mbalimbali ni miongoni mwa mambo yatakayopewa uzito.
Wahadhiri, wasomi na wanafikra mbalimbali wa masuala ya kidini na kijamii kutoka nchi tofauti za dunia watashiriki katika kongamano hilo. 654525
captcha