IQNA

Vijana wa Kiislamu wa Uturuki wagawa Qur’ani kati ya watalii wa Kikristo

0:42 - September 20, 2010
Habari ID: 1997238
Vijana wa Kiislamu wa mji wa Istanbul nchini Uturuki wamegawa kitabu cha Mwenyezi Mungu Qur’ani Tukufu kati ya watalii wa Kikristo ikiwa ni katika kulalamikia kuchomwa moto Qur’ani nchini Marekani.
Wanachama wa Idara ya Vijana ya chama cha Saadat cha Uturuki walihudhuria katika medani ya Sultan Ahmad mjini Istanbul na kutoa zawadi ya tarjumi ya Qur’ani kwa lugha ya Kiingereza kwa watalii wa kigeni.
Kundi la vijana hao hamsini lilikusanyika katika medani hiyo likiwa na vitambaa vyenye maandishi: “Soma Qur’ani, Usiichome” na kueleza upinzani wake dhidi ya kitendo cha kuchomwa moto Qur’ani nchini Marekani.
Ihsan Sorar ambaye ni miongoni mwa maafisa wa Idara ya Vijana ya chama cha Saadat alihutubia mkusanyiko huo akisema kuwa serikali ya Marekani imehalalisha kuikalia kwa mabavu Afghanistan na kuua maelfu ya watu nchini humo kwa kisingizio cha matukio ya Septemba 11 na sasa kitabu cha Mwenyezi Mungu kinachomwa moto nchini humo kwa kutumia kisingizio kingine.
Ameongeza kuwa ulimwengu unapaswa kuelewa ujumbe wa amani wa Qur’ani na kusoma kitabu hicho na baadaye kuzungumzia yaliyomo.
Baadaye nakala za tarjumi ya Kiingereza za Qur’ani tukufu ziligawanywa kati ya watalii ambao walikaribisha na kufurahishwa na hatua hiyo. 657981
captcha