IQNA

Mkuu mpya wa Baraza Kuu la Waislamu wa Ujerumani achaguliwa

17:09 - September 21, 2010
Habari ID: 1998851
Aiman Mazyek amechaguliwa na Baraza Kuu la Waislamu wa Ujerumani kusimamia shughuli za baraza hilo.
Kwa mujibu wa tovuti ya Muhit, Mazyek alifanikiwa kushinda uchaguzi huo uliofanyika siku ya Jumamosi tarehe 18 Septemba baada ya kumshinda mwenzake Ayub Excel Kohler mwenye asili ya Ujerumani.
Hata hivyo Kohler ataendelea kushirikiana na idara ya uongozi wa baraza hilo pamoja na kuwa mmoja wa washuri wakuu wa sekretarieti ya baraza hilo.
Mara tu baada ya kuchaguliwa kuongoza baraza hilo, Mazyek amesisitiza kuwa jukumu lake la kwanza litakuwa ni kuimarisha umoja wa Waislamu wa Ujerumani pamoja na utendaji wa baraza hilo. Ameongeza kuwa usimamiaji wa shughuli za mafunzo ya Kiislamu katika shule za Ujerumani na kuimarisha ushirikiano wa jamii ya wachache ya Kiislamu nchini humo ni majukumu yake mengine muhimu katika siku zijazo. 659646
captcha