Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Kuwait KUNA, mara tu baada ya kujitoa kwenye chama cha Liberal, Voorhoeve amejiunga na chama cha Liberal Democratic cha Uholanzi ambacho kinapinga vikali misimamo ya chuki na ubaguzi ya Wilders dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Kabla ya hapo, Abraham 'Ab' Klink Naibu Mwenyekiti wa chama cha Christian Democratic Party cha Uholanzi ambaye pia ni Waziri wa Afya wa nchi hiyo alikuwa tayari amejiondoa katika chama hicho akilalamikia uamuzi wake wa kujiunga na chama cha Wilders.
Chama chenye uadui mkubwa dhidi ya Uislamu cha Uhuru, Libera na Christian Democrati vimeamua kuungana kwa ajili ya kujipatia nafasi nzuri ya kisiasa nchini Uholanzi. 660160