Ukurasa wa intaneti wa prnews umeripoti kuwa mtandao huo ambayo umepewa jina la MuslimResponse.com utakuwa na jukumu la kukosoa maneno yasiyofaa yanayotumiwa kuhusiana na Waislamu na itikadi za Kiislamu kote duniani.
Mtandao huo ambao una wanachama katika nchi za Canada na Marekani, unafanya jitihada za kutoa vyanzo sahihi kwa wasomaji wake kuhusu masuala ya dunia ya leo hususan yale yanayohusiana na ulimwengu wa Kiislamu na Waislamu.
Mtandao huo una kona iliyopewa jina la 'Mtazamo Wetu' ambayo inatoa taswira sahihi ya Waislamu na mitazamo yao kuhusu matukio mbalimbali muhimu yanayohusiana na Uislamu.
Mjadala wa kwanza wa mtandao huo ni kuwazindua watu kuhusu njama ya siku ya kuchoma moto Qur'ani iliyotangazwa na kasisi wa Kimarekani. Mjadala huo unachunguza sababu za suala hilo na kutoa elimu na maarifa ya Qur'ani kwa ajili ya kuzuia hatua kama hizo.
Katika siku zijazo, mtandao wa MuslimResponse pia utakuwa ukichunguza na kuchambua matukio muhimu ya kila siku kuhusu Uislamu na Waislamu. 660563