Kwa mujibu wa tovuti ya dna, Musawi ambaye alikuwa katika mji huo kwa lengo la kuhudhuria karamu ya kila mwaka inayoandaliwa katika msikiti mkuu wa mji huo alionana na kuzungumza na viongizo hao akiwemo Askofu Mkuu Jean Pierre Galt wa Strasbourg. Pia amekutana na gavana wa mji huo na viongozi wa makanisa ya Kikristo, Kiyahudi na Kibudha na kujadiliana nao masuala mbalimbali ya kuimarisha uhusiano wa dini tofauti.
Karamu ya chakula cha jioni huandaliwa kila mwaka na Msikiti Mkuu wa Strasboug ambapo wanazuoni na wanafikra wa Kiislamu na wasiokuwa Waislamu, wawakilishi wa jumuiya na mashirika mbalimbali ya Kiislamu pamoja na viongozi wa dini tofauti za Strasbourg hujumuika kwa madhumuni ya kunyanyua kiwango cha utamaduni wa kuvumiliana na kuimarisha mazungumzo baina ya wafuasi wa dini tofauti. 660936