Brice Hortefeux Ijumaa ya jana alimtumia barua Muhammad Musawi Mkuu wa Baraza la Waislamu la Ufaransa (CFCM ) akilaani kitendo cha baadhi ya watu cha kuvunjia heshima makaburi ya Waislamu katika mji wa Strasbourg.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa amesema kuwa amesikitishwa mno na tukio hilo la kijinga na ametoa ahadi ya kutumia uwezo wake kuwatia nguvuni watu waliohusika na uhalifu huo.
Katika sehemu nyingine ya barua yake, Waziri Brice Hortefeux amewataka maafisa wa polisi ya mji wa Strasbourg kuwakamata na kuwafikisha mbeye ya vyombo vya sheria watu waliohusika na uhalifu huo.
Ni vyema kukumbusha kuwa watu wasiojulikana Alkhamisi iliyopita waliingia katika eneo la makaburi ya Waislamu wa mji wa Strasbourg na kuchora alama zinazopinga Uislamu juu ya makaburi hayo na kuvunja baadhi yao. 661966