Wito huo umetolewa baada ya Israel kulitaka baraza hilo kukomesha uchunguzi wake kuhusu jinai zilizofanywa na jeshi la utawala huo haramu katika eneo hilo la Palestina.
Nchi 57 wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC zimesisitiza katika mkutano huo kwamba Baraza la Haki za Binadamu na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa zinapaswa kudumisha uchunguzi kuhusu siasa za kihasama za utawala wa Kizayuni wa Israel katika Mashariki ya Kati.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa wiki iliyopita ilisisitiza kuwa uchunguzi uliofanyika kuhusu vita vya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza hautoshi na kwamba utawala wa Kizayuni hauonyeshi ushirikiano katika uchunguzi huo.
Katika mashambulizi yake ya mwaka jana dhidi ya Ukanda wa Gaza, Israel ilitekeleza mauaji dhidi ya raia wasiopungua 1400, thuluthi yao wakiwa watoto wadogo. Wapalestina wengine 5300 walijeruhiwa katika mashambulizi hayo.
Ripoti ya kutafuta ukweli ya Umoja wa Mataifa iliyotembelea eneo la Ukanda wa Gaza pia imesema kuwa utawala haramu wa Israel ulitekeleza jinai za kivita na kukiuka sheria za haki za binadamu. 664531