Kwa mujibu wa gazeti la nchi hiyo la ar-Rai mashindano hayo yaliandaliwa na Wizara ya Ulinzi ya Kuwait kwa ushirikiano wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya nchi hiyo.
Washindi wa mashindano hayo wataiwakilisha Kuwait katika mashindano ya kimataifa ya wanajeshi ya kuhifadhi na kusomaji Qur'ani ambayo yamepangwa kufanyika baadaye huko nchini Saudi Arabia.
Abdul Aziz ar-Rais, Mkuu wa Idara ya uongozi wa kimaanawi na uhusiano wa umma wa Wizara ya Ulinzi ya Kuwait amesema kuwa idadi kubwa ya maafisa wa jeshi walishiriki katika mashindano hayo.
Mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani maalumu kwa wanajeshi hufanyika kila mwaka nchini Saudi Arabia. Washiriki wa mashindano hayo hupata fursa ya kubadilishana uzoefu wao katika masuala ya usomaji Qur'ani na thamani za kimaadili na maarifa ya Kiislamu. 666857