IQNA

Malalamiko dhidi ya filamu inayomkosea heshima Mtume Mtukufu (saw)

13:52 - October 09, 2010
Habari ID: 2009066
Wito wa Chuo Kikuu cha Absala cha Sweden kwa Lars Felix mchorakatuni wa nchi hiyo aonyeshe katika chuo hicho filamu inayomdhalilisha Mtume Mtukufu (saw) umeamsha hasira ya Waislamu wa nchi hiyo.
Katika taarifa, chuo hicho kimesema kuwa kitashirikiana na vyombo vya usalama vya nchi hiyo kuhakikisha kuwa ulinzi mkali unawekwa wakati wa kuonyeshwa filamu hiyo.
Katika upande wa pili, Waislamu wa Sweden wamelalamikia vikali jambo hilo na kuyataka mashirika na jumuiya za Kiislamu, tasisi za Kimataifa na Waislamu wote duniani kufanya kila liwezekanalo ili kuzuia kuonyeshwa kwa filamu hiyo ya kibaguzi dhidi ya Mtume Mtukufu (saw). Wakati huohuo, Muhammad Shadi Kiskin, Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Sayansi na Utamaduni ya Sweden, amekituhumu Chuo Kikuu cha Absala kwa kuanzisha vita vichafu dhidi ya Uislamu na Waislamu, dharau dhidi ya matukufu na nembo za Kiislamu na kuchochea ghasia na dhulma dhidi ya Waislamu walio wacache wa nchi hiyo.
Amesema chuo hicho kimeanzisha vita na dhulma dhidi ya Waislamu ambao dhambi yao ya pekee ni kukiri kwamba Mungu wao wa pekee ni Mwenyezi Mungu. 670494
captcha