Wakurugenzi na wawakilishi wa mashirika ya idhaa na televisheni za Kiislamu wanachama wa Muungano wa Idhaa na Televisheni za Kiislamu kutoka nchi mbalimbali za dunia wanashiriki katika kikao hicho cha siku tatu.
Katika kikao cha ufunguzi, Ali Karimiyan, Katibu Mkuu wa muungano uliotajwa, Ali Akbar Wilayati, Mshauri Mkuu wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na Ayatullah Sheikh Asif Muhsini, mmoja wa wanazuoni mashuhuri wa kidini wa Afghanistan wamebainisha umuhimu wa vyombo vya habari katika kuakisi matukio na hali ya sasa ya ulimwengu wa Kiislamu pamoja na udharura wa kutetewa maslahi na matukufu ya Kiislamu.
Katika kikao hicho cha ufunguzi, Ismail Haniyya Waziri Mkuu wa Palestina pia amezungumzia umuhimu wa vyombo vya habari katika kuimarisha moyo wa mapambano wa wanaharakati wa Kiislamu wa Palestina katika kukabiliana na jinai za Wazayuni.
Maonyesho ya pili ya soko la filamu za Kiislamu na uwezo wa Iran katika kutengeneza zana na vifaa vya utangazaji habari yanaendelea pambizoni mwa kikao hicho. 671992