IQNA

Mamufti wa Russia wawasilisha mashtaka dhidi ya kufungwa njia za kuingia kwenye msikiti wa Moscow

14:39 - October 12, 2010
Habari ID: 2011556
Baraza la Mamufti wa Russia limewasilisha mashtaka dhidi ya uamuzi wa kuwafungia Waislamu njia za kuelekea kwenye msikiti mkuu wa Moscow.
Mashtaka hayo yamewasilishwa katika ofisi na mwendesha mashtaka wa serikali ya Russia.
Afisa wa kitengo cha habari cha Baraza la Mamufti wa Russia amesema kuwa Polisi ya nchi hiyo tangu Ijumaa iliyopita ilifunga njia kuu za kuelekea kwenye msikiti mkuu wa Moscow na imewalazimisha watu kutumia treni. Amesema kuwa hatua hiyo imewafanya watu wanaokwenda kuswali msikitini hapo washindwe kutumia njia za kando ya msikiti huo, suala ambalo limezusha ghasia na machafuko.
Amesema kuwa njia hizo zimefunguliwa baada ya swala lakini polisi ya Moscow haikuwaomba radhi Waislamu hao.
Msemaji wa polisi ya Moscow amedai kuwa idadi kubwa ya Waislamu wanakwenda katika msikiti huo kutekeleza ibada za kidini, suala ambalo linavuruga nidhamu ya mji huo. 673558
captcha