Waziri wa Elimu wa Ujerumani ambaye alikuwa akizungumzia Uislamu na wahajiri wa Kiislamu nchini humo amesema kuwa haikubaliki kwa baadhi ya watu kupinga matamshi ya Rais Christian Wulff aliyesema kuwa Waislamu ni sehemu ya jamii ya Ujerumani.
Waziri Annette Schavan ameongeza kuwa: "Zaidi ya Waislamu milioni nne wanaishi nchini Ujerumani, kuna maelfu ya misikiti na vituo vya ibada vya Kiislamu nchini humo na masomo ya Kiislamu pia yanatolewa katika shule na vyuo vikuu vya Ujerumani; kwa msingi huo Uislamu ni sehemu ya jamii ya nchi hii."
Waziri wa Elimu wa Ujerumani amesema anatarajia kuwa nchi za Kiislamu zitafanya jitihada za kustawisha utamaduni wa mazungumzo kati ya dini mbalimbali katika nchi hizo.
Kuhusu mtazamo wake juu ya vazi la staha la mwanamke wa Kaiislamu hijabu, Waziri Annette Schavana amesema kuwa kwa mujibu wa sheria za Ujerumani hakuna tatizo lolote kwa mwanamke mwenye vazi la hijabu kuhudhuria katika shughuli za kijamii na kwamba yeye binafsi hapingi suala la kuwepo wanawake wenye vazi hilo katika Wizara ya Elimu ya Ujerumani. 673598