IQNA

Kikao cha Ulimwengu wa Kiislamu na Udhibiti wa Vyombo Habari kinafanyika leo

15:30 - October 13, 2010
Habari ID: 2012388
Kikao cha kitaalamu kinachobeba anwani ya 'Ulimwengu wa Kiislamu na Udhibiti wa Vyombo vya Habari' kinafanyika leo Jumatano katika maonyesho ya nne ya kimataifa ya Vyombo vya Habari vya Digitali mjini Tehran. Kikao hicho kinahudhuriwa na wakurugenzi wa Jamiatul Mustafa al Alamiyya na Prf. Suhail As'ad.
Prf. Suhal As'ad kutoka Argentina ambaye amehitimu masomo katika Jamiatul Mustafa al Alamiyya atatoa hotuba katika kikao hicho akizungumzia maudhui ya Ulimwengu wa Kiislamu na Udhibiti wa Vyombo vya Habari.
Wakati huo huo msimamizi wa chumba cha Jamiatul Mustafa al Alamiyya katika maonyesho ya kimataifa ya vyombo vya habari vya digitali amesema Prf As'ad ni mhubiri mahiri wa Kiislamu ambaye ana uzoefu wa kufundisha katika vyuo vikuu 80 na anaweza kuzungumza kwa kutumia lugha za Kihispania, Kiingereza, Kiarabu na Kifarsi. 674435
captcha