IQNA

Njia za kunyanyua kiwango cha elimu na utafiti katika nchi za Kiislamu zachunguzwa

12:46 - October 14, 2010
Habari ID: 2012660
Njia za kunyanyua kiwango cha elimu na utafii kwa madhumuni ya kuimarisha nchi za Kiislamu katika nyanja hizo zitachunguzwa katika kikao cha Mawaziri wa Elimu wa nchi hizo kinachotazamiwa kufanyika kati ya tarehe 19 hadi 21 za mwezi huu wa Oktoba huko nchini Malaysia.
Kwa Mujibu wa Shrika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO, kikao cha tano cha Mawaziri wa Elimu ya Juu na Utafiti wa Kielimu wa Nchi za Kiislamu ICMHESR kitafanyika tarehe zilizotajwa huko Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia.
Uundwaji wa jumuiya ya wanawake wasomi wa Kiislamu na katiba yake, kuwasilishwa ripoti ya Katibu wa Jumuiya ya Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu kuhusiana na shughuli za jumuiya hiyo tokea ianzishwe hadi leo na vilevile ripoti ya Katibu Mkuu wa ISESCO kuhusu jambo hilo ni masuala yatakayojadiliwa katika kikao cha Kuala Lumpur.
Maendeleo ya teknolojia ya kisasa na nafasi ya wanawake wa Kiislamu katika uwanja huo ni mambo mengine yatakayochunguzwa katika kikao hicho.
Mahathir Muhammad, Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia ambaye pia ni mjumbe wa mazungumzo baina ya tamaduni na staarabu wa ISESCO ni mmoja wa watu watakaohutubia kikao hicho cha mawaziri. 673907
captcha