Kongamano hilo la siku tatu litahudhuriwa na wasomi pamoja na wanafikra mashuhuri wa Kiislamu na wasiokuwa Waislamu ambapo watachunguza masuala mbalimbali yakiwemo ya iwapo Uislamu unaambatana na baadhi ya tamaduni za Ulaya au la.
Thamani za Kiislamu, Uislamu na demokrasia, Uislamu na mwanamke, Uislamu na ukisasa, Uislamu na vyombo vya habari, mazungumzo kati ya dini tofauti, Uislamu katika vitabu vya masomo na kuenezwa chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi ni masuala mengine yatakayochunguzwa katika kongamano hilo. 679194