IQNA

Kuhani wa Kizayuni ataka Wapalestina watumiwe kama ngao ya kibinadamu

13:42 - October 23, 2010
Habari ID: 2017627
Kuhani mmoja wa Kizayuni ametoa fatuwa yenye utata mkubwa akitaka Wapalestina watumiwe na jeshi la utawala wa Kizayuni kama ngao ya kibinadamu.
Kwa mujibu wa tovuti ya Lubnan al-Aan, Kuhani Is'haq Shaibra ambaye ni mmoja wa makuhani wenye misimamo ya kupindukia mipaka wa Kizayuni ametoa fatuwa hiyo ya kijinai akiwaruhusu askari wa Kizayuni kuwatumia Wapalestina kama ngao ya kibinadamu katika operesheni zao za kijeshi. Kuhani huyo muovu mwaka mmoja uliopita pia aliandika kitabu kilichowaruhusu Mayahudi kuua raia wa Kipalestina wasio na hatia wakiwemo watoto wadogo. 679993
captcha