IQNA

Muungano wa Uturuki na Uislamu barani Ulaya waunga mkono matamshi ya Rais wa Ujerumani kuhusu Uislamu

11:46 - October 24, 2010
Habari ID: 2018448
Selahattin Saygın, Katibu Mkuu wa Muungano wa Uturuki na Uislamu barani Ulaya ameunga mkono matamshi yaliyotolewa hivi karibuni na Rais Christian Wulff wa Ujerumani kuhusu Uislamu.
Saygin amesema Waislamu wanaunga mkono matamshi ya kiongozi huyo aliyesema kuwa rais wa Ujerumani pia ni rais wa Waislamu wa nchi hiyo na kuongeza kuwa, Waislamu wa Ujerumani vilevile wanamtambua kiongozi huyo kuwa rais wao. Amesema, matamshi ya Rais Wulff kuwa Uislamu ni sehemu ya Ujerumani na hatua yake ya kuitembelea Uturuki katika mazingira magumu ya hivi sasa ambapo Waislamu wamekuwa wakishambuliwa na maadui tokea kila upande ni jambo ambalo limewapa Waislamu matumaini ya kuimarika nafasi yao nchini humo.
Amesema marais wa zamani wa Ujerumani waliwahi pia kutoa matamshi kama hayo lakini hawakuwahi kukabiliwa na ukosoaji kama huu unaotolewa dhidi ya rais wa hivi sasa wa nchi hiyo.
Saygin amesisitiza kwamba ukosoaji na hujuma ya maadui dhidi ya matamshi hayo ni jambo ambalo limeiweka serikali ya Ujerumani katika nafasi tata ya kutetea kwa uadilifu haki za raia wake wote na hasa Waislamu wanaokabiliwa na hujuma ya maadui wa Uislamu nchini humo. Ameongeza kuwa safari ya Rais Wulff nchini Uturuki imeongeza matumaini ya wahajiri wa Uturuki nchini Ujerumani na kwamba itaimarisha zaidi mazingira ya raia hao kuishi pamoja kwa amani na raia wenzao wa Ujerumani. 680630
captcha