Nchi za Kenya, Iraq, Tajikistan, Uturuki, Argentina, China, Syria, Ufaransa, Palestina zilishiriki katika siku ya kwanza ya ufunguzi wa maonyesho hayo. Nchi nyingine za Tanzania, Uingereza, Albania, Belarus, India, Croatia, Misri, Lebanon, Korea Kusini, Yemen, Qatar, Libya, Georgia, Kuwait, Kyrgyzstan na Russia zinatazamiwa kushirikia katika maonyesho hayo tokea leo Jumanne.
Maonyesho ya 17 ya kimataifa ya magazeti na mashirika ya habari ya mjini Tehran yataendelea hadi siku ya Jumatatu tarehe Mosi Novemba. 682704