Mkuu wa Msafara wa Hija wa Iran akutana na mwenzake wa Senegal
Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya Hija ambaye pia ni Mkuu wa Msafara wa Iran katika Hija amekutana na Amirul Haj (Kiongozi wa Mahujaji) wa Senegal katika Mji Mtakatifu wa Madina.
Katika Mkutano huo Hujjatul Islam Ghazi Asghar Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya Hija amesifu uhusiano mzuri wa Iran na Senegal.
Amesema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na Rais Mahmoud Ahmadinejad wanalipa umuhimu suala la kuimarisha uhusiano na nchi za Kiafrika hasa Senegal.
Amirul Haj wa Senegal ametaka uimarishwe uhusiano wa Iran na Senegal hasa katika masuala ya Hija.
682921