IQNA

Propaganda chafu dhidi ya Uislamu ni alama ya woga wa Wamagharibi kuhusu Uislamu

15:50 - November 02, 2010
Habari ID: 2024386
Maendeleo makubwa ya dini ya Kiislamu katika nchi za Magharibi na mvuto wa mafundisho halisi ya Mtume Muhammad (saw) yamewafanya maadui wa dini hiyo kuanzisha wimbi la propaganda za kuchafua jina la Uislamu.
Hayo yamesemwa na Assane Samb, mhariri msaidizi wa gazeti la Lematindafrique na mwakilishi wa Senegal katika Maonyesho ya Kimataifa ya Magazeti na Vyombo vya Habari mjini Tehran.
Assane Samb amesema kuwa licha ya njama kubwa zilizofanywa na maadui wa Uislamu lakini hawajafanikiwa kusimamisha kasi ya dini hiyo katika nchi za Magharibi.
Ameongeza kuwa matukio ya kuchomwa Qur'ani nchini Marekani ni sehemu ya siasa za kupiga vita ustaarabu wa Kiislamu. Amesema kuwa woga wa Wamagharibi kuhusu kasi ya dini ya Kiislamu umewafanya hata viongozi wa Kikristo kama Terry Jones kuanzisha vita dhidi ya Uislamu na kwamba njama kama hizo haziwezi kufanikiwa.
Mhariri msaidizi wa gazeti la Lematindafrique amesema kuwa propaganda chafu dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi hazilengi dini ya Kiislamu pekee bali utamaduni mzima wa wafuasi wa dini hiyo, tamaduni za Kiyahudi na wa Kikristo. 684889
captcha