IQNA

Kikao cha Kimataifa cha Quds chafanyika Ghaza

14:00 - November 06, 2010
Habari ID: 2026324
Kikao cha Nne cha Kimataifa cha Taasisi ya Kimataifa cha 'Quds' kimefanyika katika Ukanda wa Ghaza kwa lengo la kuchunguza njama haribifu za Utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Quds hasa kuuyahudisha mji huo.
Washiriki katika kikao hicho wametaka kuwepo jitihada zaidi za madola ya Kiislamu katika kukabiliana na hujuma za kinyama za Wazayuni hasa katika kuuyahudisha mji wa Quds Tukufu.
Akizungumza katika kongamano hilo, Mushir al Masri Mwakilishi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas katika Bunge la Palestina amesema kuwa ,'ufa na migawantyiko miongoni mwa makundi ya Kipalestina ni hatari kubwa inayotishia malengo ya Wapalestina hasa ya kuikomboa Quds Tukufu'. Amesema hii ndio sababu anwani ya kikao hicho ikatajwa kuwa 'Umoja kwa Ajili ya Quds, Al Aqsa na Matukufu'.
689094
captcha