IQNA

16:01 - November 06, 2010
Habari ID: 2026445

Ufaransa kuwa mwenyeji wa kikao cha 'Ziara katika Uislamu na Ukristo'

Kikao cha Ziara katika Uislamu na Ukristo kimepangwa kufanyika tarehe 4 Disemba katika mlolongo wa wiki ya kumi ya mazungumzo kati ya Uislamu na Ukristo katika mji wa Paris nchini Ufaransa.

Kituo cha habari cha Semaineseric kimeripoti kuwa msikiti mkuu wa Paris, Kundi la Urafiki kati ya Uislamu na Ukristo (GAIC), Jumuiya ya Misaada ya Kiislamu ya Ufaransa, Kamati ya Kupambana na Umaskini na Njaa na Jumuiya ya Sayansi na Teolojia ya Taasisi ya Kikatoliki ya Paris (ISTR) zinashirikiana katika kuandaa kikao hicho.
Kikao hicho kitafunguliwa kwa hotuba ya mwenyekiti wa msikiti mkuu wa Paris Dalil Bubakr na washiriki watazungumzia maudhui mbalimbali kama 'ziara, njia mpya ya mazungumzo', 'mambo ya pamoja ya ziara katika dini za Kiislamu na Kikristo', 'ziara katika Uislamu', 'hija, umra na maeneo matakatifu', 'ziara katika Ukristo, Baitul Muqaddas na maeneo matakatifu nchini ufaransa.
Mkutano huo utahudhuriwa na shakhsia wa kidini na kisiasa nchini Ufaransa. 689296


captcha