Hassan Chalghumi ambaye alikuwa akihutubia katika kituo cha Mayahudi mjini Lyon ameeleza wasiwasi wake mkubwa juu ya ongezeko la makundi yenye misimamo mikali ya Kiwahabi nchini Ufaransa na akasema kuwa kunawatia wasiwasi Waislamu wote wa Ufaransa.
Hata hivyo amesema kuwa Uislamu unaendelea kustawi nchini Ufaransa licha ya propaganda chafu zinazofanywa dhidi ya dini hiyo tukufu.
Amesema njia pekee ya kukabiliana na fikra za Kiwahabi na makundi potofu ni kuteuwa maimamu wa misikiti kutoka ndani ya Ufaransa kwenyewe ni si kuchukua maimamu hao kutoka nje ya nchi. 691768