Kwa mujibu wa tovuti ya Dunyabulteni Baraza la Waislamu la Ujerumani limetaja hatua ya taasisi ya Friedrich Naumann inayofungamana na chama chenye misimamo ya chuki dhidi ya Uislamu cha Liberal Democrat FDP ya kumtunuku zawadi mtu huyo kuwa ni hatua moja nyuma katika juhudi za kuwaunganisha Waislamu wa Ujerumani na jamii ya nchi hiyo.
Aiman Mazyek, Mkuu wa Baraza la Waislamu la Ujerumani amesema kuhusiana na suala hilo kwamba kutunukiwa zawadi ya uhuru wa kusema Necla Kelek, mtu ambaye ni mashuhuri kwa kutoa matamshi yaliyo dhidi ya Uislamu nchini Ujerumani hakuna lengo jingine isipokuwa kuzidisha mvutano kati ya Waislamu na wasio Waislamu wa nchi hiyo. Amesema hatua hiyo bila shaka itaongeza dhana mbaya nchini Ujerumani kuhusiana na Uislamu na kwamba hilo ni jambo linalokwenda kinyume na juhudi zinazofanywa na serikali kwa lengo la kuwaunganisha Waislamu katika jamii ya nchi hiyo.
Makundi mengine ya Kiislamu ya Ujerumani likiwemo lile linalounga mkono Chama cha Kijani cha nchi hiyo pia yamelaani vikali hatua hiyo ya kutunukiwa zawadi ya uhuru wa kujieleza Necla Kelek. 693187