Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiisamu ISESCO siku ya Jumanne lilitiliana saini mkataba wa kuimarisha ushirikiano na Baraza la Uhusiano wa Jumuiya za Kiislamu za Marekani CAIR huko Rabat, mji mkuu wa Morocco.
Mkataba huo ulitiwa saini na Abdul Aziz Othman al Tuwaijri, Katibu Mkuu wa ISESCO na Nahad Awadh, Mkurugenzi Mwandamizi wa CAIR.
Kuimarishwa uhusiano wa pande mbili katika nyanja za utamaduni na mazungumzo baina ya dini na tamaduni, kushughulikiwa masuala ya Waislamu katika nchi za Ulaya, kupambana na chuki dhidi ya Uislamu, mapambano dhidi ya ubaguzi wa kidini, ushirikiano katika kuelimisha vijana wa Kiislamu na kuarifishwa vyema Uislamu kupitia vyombo vya habari na vitabu vya masomo ni baadhi ya mambo yaliyoafikiwa katika mkataba huo.
Shirika la ISESCO pia siku ya Jumanne lilitiliana saini mkataba kama huo na Kituo cha Utafiti na Maelezo cha Waarabu cha mjini Washington. 692991