Kwa mujibu wa gazeti la Al Rai, mpango huo unatokana na ile hadithi ya Mtume SAW aliposema: "Mbora wenu ni yule anayejifunza na kuwafunza wengine Qur'ani'.
Sabah al Yakub, mwanachama wa Taasisi ya Misaada ya Al Najat amesema kuwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, Kuwait imetoa mchango mkubwa katika sekta ya masomo ya Qur'ani. Amesema taasisi yake inajitahidi kutekeleza mpango wa 'Khairukum' ili kutoa mafunzo ya kimsingi ya Qur'ani kwa wanafunzi 2000 wa vyuo vikuu.
"Qur'ani Tukufu inatuonyesha njia sahihi, ni msingi wa tauhidi na chuimbuko asili la sheria za Kiislamu, hekima na malengo ya Mitume", amesema.
695885