Kwa mujibu wa tovuti ya medyaradar, Cihan Aktas mwandishi mashuhuri Muislamu wa kike wa Uturuki amejiondoa katika kikao hicho cha Bunge la Waandishi la Ulaya ambacho kimepangwa kufanyika mjini Istanbul tarehe 25 hadi 27 Novemba ikiwa ni alama yake ya kulalamikia kualikwa kwa mwandishi huyo mwenye asili ya Uingereza katika kikao hicho.
Cihan Aktas ambaye alikuwa amepangiwa kuhutubia kikao hicho amesema amejiondoa katika kikao hicho kutokana na kualikwa kwa mwandishi huyo wa Uingereza katika kikao hicho cha Bunge la Waandishi la Ulaya kama mgeni wa heshima.
Wakati huohuo, Hilmi Yavuz mwanafalsafa na mshairi mashuhuri wa Uturuki amekosoa vikali kualikwa katika kikao hicho mwandishi huyo anayekosea heshima Uislamu na Waislamu.
Kikao cha Istanbul kinafanyika katika fremu ya kutangazwa mji huo kuwa mji mkuu wa kiutamaduni wa Ulaya katika mwaka huu wa 2010. Mwaka 2001 Naipaul aliushutumu vikali Uislamu na Waislamu na kuituhumu dini hii tukufu ya mbinguni kuwa ya kikoloni! 699637