Akizungumza mjini Beirut, Erdogan amehoji kwamba "Je, Israel inafikiri kuwa itaingia Lebanon kwa ndege zake za kisasa na mabuldoza na kuuwa wanawake na watoto, kuharibu shule na mahospitali huku ikitegemea kuwa tutanyamaza kimya?". Kwa hakika hatutanyamaza kimya na tutaunga mkono uadilifu kupitia njia zote zinazowezekana!" amesisitiza Recep Tayyip Erdogan. Pia Waziri Mkuu wa Uturuki ameongeza kwamba, utawala haramu wa Israel utashindwa kama ulivyoshindwa huko nyuma.
Uturuki ilikuwa mshirika wa karibu wa kijeshi na kidiplomasia wa utawala wa Kizayuni wa Israel, lakini uhusiano wa pande hizo mbili ulianza kuharibika miezi kadhaa iliyopita baada ya makomandoo wa Israel kushambulia meli ya misaada ya kibinadamu kwa ajili ya raia Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza na kuwaua wanaharakati kadhaa wa Uturuki.
701735