Kikao hicho ambacho kitahudhuriwa na viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) kitajadili changamoto zinazoukabili umma wa Kiislamu na kuchukua maamuzi ya jinsi ya kutatua matatizo hayo.
Masuala mengine yatakayojadiliwa katika kikao hicho ni hali ya mambo nchini Afghanistan na rasimu iliyowasilishwa katika Umoja wa Mataifa ya azimio la kupiga marufuku dharau na kuvunjiwa heshima matukufu ya kidini.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Misri kuwa mwenyeji wa viongozi wa nchi Kiislamu na kwa hatua hiyo inataka kuonyesha uungaji mkono wake kwa shughuli za pamoja za Kiislamu na umoja kati ya nchi za Kiislamu katika masuala ya kisiasa, kiuchumi na masuala ya ustawi.
Kikao cha viongozi wa nchi za Kiislamu hufanyika mara moja kila baada ya miaka mitatu katika mojawapo ya nchi wanachama.
Kikao cha kwanza kabisa cha viongozi wa OIC kilifanyika mwaka 1969 mjini Rabat, Morocco na cha mwisho kilifanyika yapata miaka mitatu iliyopita katika mji mkuu wa Senegal, Dakar. 703833