Sherehe ya kumalizika maadhimisho ya Moroni, mji mkuu wa visiwa vya Comoro, kuwa mji mkuu wa kiutamaduni wa ulimwengu wa Kiislamu barani Afrika katika mwaka huu wa 2010 imeanza leo Jumanne.
Wawakilishi wa Shrika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO wanahudhuria sherehe hiyo maalumu itakayoendelea kwa muda wa siku nne.
Katika maadhimisho hayo, Isesco inashirikiana na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO kutoa mafunzo maalumu kwa maafisa wa Comoro kuhusu masuala ya kiutamaduni. Ratiba maalumu zinazohusiana na masuala ya kiutamaduni yakiwemo ya michezo ya kiugiza, kutembelea majengo ya kale ya turathi za Kiislamu na pia kuenziwa watu waliokuwa na taathira katika kuhuisha utamaduni wa Kiislamu mjini Moroni zitatekelezwa katika maadhimisho hayo.
Ni muhimu kukumbusha hapa kuwa miji ya Tarim nchini Yemen na Dushanbe mji mkuu wa Tajikistan ilichaguliwa na ISESCO kuwa miji mikuu ya kiutamaduni ya Kiislamu katika ulimwengu wa Kiarabu na bara Asia kwa utaratibu katika mwaka huu wa 2010. 704293