Shirika la habari la Indonesia Bernama limeripoti kuwa Waziri wa Masuala ya Kidini wa nchi hiyo Suryadharma Ali amesema kuwa kwa sasa nchi kama Russia, Vietnam, Cambodia, Mianmar na Thailand zinashirikiana na nchi yake katika masuala yanayohusu dini ya Kiislamu.
Ameongeza kuwa Wizara ya Masuala ya Kidini ya Indonesia pia inashirikiana na jamii za Kiislamu kutoka nchi mbalimbali duniani katika masuala ya hija, elimu, ulinganiaji wa Kiislamu na kupambana na ugaidi.
Waziri Suryadharma Ali amesema Indonesia inatoa nafasi za masomo ya Kiislamu kwa wanafunzi kutoka Russia na imetuma wahubiri wa Kiislamu katika miji 40 mikubwa ya Russia. 704693