Kongamano hilo linahudhuriwa na shakhsia 1000 kutoka taasisi 100 zinazojihusisha na masuala ya mateka na pia wawakilishi wa jumuiya za Kipalestina, Kiarabu na kimataifa kutoka nchi 55 duniani.
Mwanafikra wa Kiyahudi anayewatetea wananchi wanaokandamizwa wa Palestina Stanly Cohen, waziri mkuu wa zamani wa Malaysia Mahathir Muhammad na rais wa zamani wa Sudan Abdul Rahman Siwar Al Dahab ni miongoni mwa shakhsia watakaohudhuria kongamano hilo. 705920