IQNA

Kutajwa Muharram kuwa mwezi wa umoja wa kitaifa na udugu nchini Kuwait

11:33 - December 06, 2010
Habari ID: 2043064
Sayyid Muhammad Baqir al-Muhri, mwakilishi wa mamarja' wa Kishia nchini Kuwait ametaka mwezi mtukufu wa Muharram uitwe mwezi wa umoja wa kitaifa na udugu wa Kiislamu nchini humo.
Akitoa taarifa katika kuwadia mwezi huu wa kwanza katika kalenda ya Kiislamu, Sayyid Muhammad Baqir al-Muhri ametaka hatua za lazima zichukuliwe kwa madhumuni ya kupambana na fikra za kuwakufurisha Waislamu, zinazoenezwa na baadhi ya watu, fikra ambazo zimeharibu jina na sura ya Uislamu duniani.
Taarifa hiyo imesema kuwa Bwana wa Mashahidi, Imam Hussein (as), aliwaunganisha Waislamu wote katika kupambana na ugaidi, dhulma, uonevu na kutetea haki, uhuru, uadilifu na demokrasia na hivyo kudhihiri kuwa kiongozi na muhubiri muhimu wa umoja katika umma wa Kiislamu.
Katika taarifa hiyo, Sayyid al-Muhri amewataka wahubiri na mubalighina wote kuongoza na kuhamasisha mwamko miongoni mwa vijana na kusisitiza udharura wa kupatikana umoja miongoni mwa madhehebu yote ya Kiislamu. Amesema kuna umuhimu wa kutenganishwa wafuasi wa madhebu ya Suni na makundi maovu ya Kiwahabi yanayowakufurisha Waislamu. Amesema Masuni wanayapinga makundi hayo na kwamba mataifa ya eneo la Mashariki ya Kati hayapasi kuchukua misimamo ya makosa inayovuruga umoja miongoni mwa Waislamu. Ametaka kutangazwa siku ya Ashura kuwa siku rasmi ya mapumziko nchini Kuwait kwa lengo la kuheshimu damu ya Imam Hussein (as) pamoja na babu yake mtukufu, Mtume Muhammad (saw). 706909
captcha