Kwa mujibu wa tovuti ya Islam Today, licha ya kuwepo matatizo na hitilafu kati ya jamii za Kiislamu na zisizo za Kiislamu za nchi hizo, lakini raia wengi wa nchi hizo wana mtazamo chanya kuhusu Waislamu. Uchunguzi huo pia unaonyesha kwamba wanachi wa Ujerumani wana mtazamo wa ukosoaji dhidi ya Uislamu na kwamba upinzani wao dhidi ya ujenzi wa misikiti nchini humo ni mkubwa zaidi ukilinganishwa na wa raia wa nchi tatu zilizotajwa. Matokeo hayo yamewashangaza watu wengi duniani kwa kutilia maanani kwamba vitendo vya kuyakosea heshima matukufu ya Kiislamu vimekuwa vikifanyika katika nchi hizo, ikiwemo marufuku ya hijabu nchini Ufaransa, uchapishwaji wa vikatuni vya dharau dhidi ya Mtume Muhammad (saw) nchini Denmark na hatua ya Geert Welders ya kutengeneza filamu ya Fitna dhidi ya Uislamu.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, asilimia 62 ya Waholanzi, 56 ya Wafaransa, 55 ya Wadenmark na asilimia 47 ya Wareno wana mtazamo chanya kuhusu Waislamu.
Matokeo hayo yanaonyesha kwamba asilimia 34 tu ya raia wa magharibi mwa Ujerumani na 26 ya wakazi wa mashariki mwa nchi hiyo ndio walio na mtazamo mzuri kuhusu Uislamu na Waislamu. Matokeo hayo yanaendelea kuonyesha kwamba kutokana na taasubi za kidini, raia wengi wa Ujerumani hawakubali kwamba Uislamu ni moja ya dini za nchi hiyo. 706869