IQNA

Tukio la Ashura lazungumziwa katika mtandao wa Jumuiya ya Ahlul Beit ya Uingereza

16:46 - December 12, 2010
Habari ID: 2046785
Jumuiya ya Ahlul Beit (as) ya Uingereza imezungumzia tukio la Ashura katika mtandao wake kama mojawapo ya njia za kubainisha na kueneza mafundisho yanayotokana na mapambano ya Imam Hussein (as) huko Karbala.
Ili kuwanufaisha watu wengi kadiri inavyowezekana, jumuiya hiyo imewataka watu wanaotembelea tovuti hiyo kusoma kwa makini mafundisho yanayotokana na mapambano hayo na kisha kuchapisha na kuyaeneza kwa watu wengine.
"Shakhsia ya kudumu milele ya Imam Hussein (as),' 'Imam Hussein; Nembo ya mapenzi na kujitolea', 'Imam Hussein (as); Kiongozi wa ulimwengu na kuvumbuliwa Uislamu' ni baadhi tu ya anwani za makala muhimu zilizoandikwa kwenye tovuti hiyo. 710932
captcha