IQNA

Jumuiya ya amani ya Uingereza yapinga safari ya kasisi wa Marekani anayekosea heshima Qur'ani

15:58 - December 13, 2010
Habari ID: 2047379
Jumuiya ya kutetea amani ya 'Matumaini Ndio, Chuki Hapana' ya nchini Uingereza imepinga vikali mwaliko wa kuitembelea nchi hiyo, uliotolewa na mrengo wa kulia kwa Kasisi Terry Jones wa Marekani ambaye hivi karibuni alizusha wimbi kubwa la malalamiko na ukosoaji duniani baada ya kutoa matamshi ya dharau dhidi ya Qur'ani Tukufu na kutaka kitabu hicho kitakatifu kiteketezwe.
Kasisi huyo amealikwa kuutembelea mji wa Luton. Huku akikosoa vikali hatua ya mrengo huo ya kumualika nchini Uingereza Terry Jones, mkuu wa jumuiya iliyotajwa amesema kuwa mrengo huo umechukua hatua hiyo kwa madhumuni ya kuchochea fikra za waliowengi na kueneza vitendo vya ghasia nchini. Amesema Jones hapasi kuruhusiwa kukanyaga ardhi ya Uingereza kwa sababu ni watu wenye misimamo ya kupindukia mipaka tu ndio watakaonufaika na safari yake nchini humo. Ameongeza kuwa watu wote wanafahamu kuwa ni mirengo kama hiyo tu ndiyo inayonufaika na fursa kama hizo za kuimarisha misimamo yao ya chuki kwa shabaha ya kueneza vitendo vya ghasia nchini. Inasemekana kuwa kundi la English Defence League lina lengo la kuandaa kikao cha kuimarisha misimamo ya kibaguzi dhidi ya Uislamu nchini Uingereza mwakani ambapo watu mashuhuri walio na chuki dhidi ya dini tukufu ya Kiislamu akiwemo Terry Jones, wamealikwa kuhutubu. 711413
captcha