IQNA

Muungano wa wanazuoni wa Palestina watahadharisha dhidi ya kuharibiwa Masjidul Aqsa

16:32 - December 13, 2010
Habari ID: 2047493
Muungano wa Wanazuoni wa Palestina LPS umetahadharisha juu ya mwenendo wa kuendelezwa shughuli za Wazayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Quds na hasa karibu na Msikiti wa al-Aqsa, jambo ambalo litapelekea kuharibiwa kwa msikiti huo mtakatifu.
Kwa mujibu wa tovuti ya Palestina Info muungano huo umetoa taarifa ukisema kuwa utawala haramu wa Israel umeanza kutekeleza mpango wa kuharibu Masjidul Aqsa na maeneo ya karibu kwa lengo la kuwaweka walowezi wa Kiyahudi katika maeneo hayo.
Umesema kuwa mataifa ya Kiislamu na Kiarabu yanapasa kukomesha kimya chao na kusimamisha haraka iwezekanavyo hatua hizo haribifu za Wazayuni.
Muungano huo pia umeeleza kushangazwa kwake na kimya cha baadhi ya nchi za Kiislamu kuhusu suala hilo. 711204
captcha